Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Geita imefanikiwa kuzuia upotevu wa zaidi ya Sh milioni 94.21 zilizokuwa zimefujwa kupitia miradi ya maendeleo na malipo haramu.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud, amewasilisha Taarifa ya Randama ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa mwaka wa fedha 2026/2027 mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU)
Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Stephen Wasira, amewatahadharisha wanachama wa chama hicho kuacha tabia ya kuanzisha mivutano na uchochezi wanapokosa fursa za uteuzi au kushindwa katika kura za maoni.
Akizungumza mkoani Geita wakati wa uwekaji wa Jiwe la msingi la Jengo la Ofisi za Mkoa, Wasira amesisitiza kuwa kukosa uongozi kusitumiwe kama kigezo cha kuvuruga amani ya Chama na Taifa, kwani kufanya hivyo ni kuhatarisha usalama wa Nchi.