MAFURIKO YAATHIRI NYUMBA 32 NA MASHAMBA KILOSA
Nyumba 32 zimeathiriwa na mafuriko huku Nyumba Sita zikibomoka kabisa pamoja na Mashamba yenye Mazao mbalimbali yakiwemo Mahindi ekari 300 yamesombwa na maji ya mafuriko katika Kijiji cha Mhenda kilichopo Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro kutokana na Mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali Wilayani humo.

