TANESCO LINDI YAONGEZA UWEZO WA KITUO CHA MAHUMBIKA KUKIDHI MAHITAJI YA UMEME

Kutokana na ongezeko la mahitaji ya Umeme katika Mikoa ya Lindi na Mtwara, Shirika la Umeme tanzania (TANESCO) Mkoa wa Lindi limeanzisha mradi wa kuongeza uwezo wa kituo cha kupooza umeme cha maumbika kwa kufunga transfoma yenye uwezo wa zaidi ya megawati 15 kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni 702.

DKT. MWIGULU AWAOMBA WATANZANIA KUENDELEA KUMUOMBEA MHE. LUKUVI

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba amewaomba Watanzania waendelee kumuombea kwa Mwenyezi Mungu aliyekuwa Waziri Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu, marehemu William Lukuvi aliyefariki jana Machi 25, 2026 katika Hospitali ya Benjamin Mkapa, jijini Dodoma.
Akiongea kwa niaba ya Serikali nyumbani kwa marehemu Area D, jijini Dodoma leo, Alhamisi, Machi 26, 2026, Waziri Mkuu amesema: “Kwa niaba ya Serikali natoa pole kwa familia, ndugu, jamaa. Jambo hili zito, gumu kulielewa, gumu kulipokea.”

HARAKATI ZA KUKITAMBUA KISWAHILI MITANDAONI ZAANZA

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Tanzania Paul Makonda, amesema Serikali imeanza mazungumzo na UNESCO pamoja na Uongozi wa Kampuni Mama inayomiliki Mitandao ya Kijamii ya Faceebok, Instagram na Whatsapp (Meta) ili lugha ya Kiswahili itambulike rasmi kwenye majukwaa ya Mitandao hiyo na kuwezesha Vijana wanaotengeneza maudhui kwa Lugha hiyo walipwe malipo makubwa kulingana na kazi zao.

Makonda ameyazungumza haya wakati wa Kongamano la 5 la Idhaa za kKswahili Duniani lililofanyika Jana Arusha.

ZRCP ELIMISHENI UMUHIMU WA MATOKEO YA TAFITI

Rais Wa Zanzibar Na Mwenyekiti Wa Baraza La Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Ameushauri Uongozi Wa Kituo Cha Tafiti Za Kiuchumi, Kijamii Na Uchambuzi Wa Sera Zanzibar –Zrcp- Kuandaa Mikutano Na Mijadala Na Wadau Ili Kuwaelimisha Kuhusu Umuhimu Wa Kutumia Matokeo Ya Tafiti Katika Utekelezaji Wa Majukumu Yao.

Ni Ziara Ya Ujumbe Wa Kituo Cha Tafiti Za Kiuchumi, Kijamii Na Uchambuzi Wa Sera Zanzibar –Zrcp- Katika Ikulu Ya Vuga Hapa Zanzibar.

DKT.NCHIMBI AAGIZA KUFANYIKA UTAFITI SEKTA YA MISITU

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Emanuel Nchimbi, ameielekeza Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na Taasisi ya utafiti wa Misitu Tanzania (Tafori) kufanya utafiti utakaosaidia kutatua matatizo mbalimbali yanayowakabili Wakulima wa Miti, hususan katika mMsitu ya asili.

Dkt. Nchimbi ametoa maelekezo hayo wakati wa ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku ya Misitu Duniani pamoja na Kampeni ya Kitaifa ya Upandaji Miti iliyofanyika katika Manispaa ya Lindi, Mkoani Lindi.

Subscribe to
 

Simplenews subscription

The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.