ZANZIBAR YAKABILIWA NA UHABA WA WATAALAMU WA USONJI

USONJI
English

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema hali ya Usonji kwa Watoto ni changamoto kubwa katika Jamii, hivyo Serikali ina wajibu wa kuhakikisha inaunga mkono jitihada za kuwasaidia Watoto wanaoathirika na hali hiyo.

Rais Mwinyi ameyasema hayo Leo, alipokutana na Viongozi wa Lukiza Autism Foundation waliomtembelea Ikulu kujitambulisha na kueleza shughuli za Taasisi hiyo,amesema kuwa tatizo la Usonji limekuwa changamoto kwa Wananchi wengi, hali inayochangiwa kwa kiasi kikubwa pamoja na ukosefu wa Elimu ya kutosha kwa Jamii pamoja na uhaba wa Wataalamu wa Fani hiyo.

Aidha, Dkt. Mwinyi ameigiza Wizara ya Afya kushirikiana na Wataalamu hao ili kujifunza zaidi kuhusu hali ya Usonji, akibainisha kuwa kwa sasa Zanzibar inakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa Wataalamu wa kutambua na kushughulikia hali hiyo mapema.

Kwa upande wake, Mtendaji Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Lukiza Autism Foundation, Hilda Nkabe, amesema kuwa bado Zanzibar inakabiliwa na changamoto nyingi katika kutambua Watoto wenye Usonji kutokana na ukosefu wa Wataalamu na vituo Maalum vya huduma hiyo.

 

Simplenews subscription

The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.