TANESCO LINDI YAPOKEA VITENDEA KAZI VYENYE THAMANI YA BILIONI 1.09 KUBORESHA HUDUMA YA UMEME

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Lindi
English

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Lindi limepokea vitendea kazi vipya vyenye thamani ya Shilingi bilioni 1.09 kwa lengo la kuboresha upatikanaji wa huduma ya umeme kwa wananchi.

Vitendea kazi hivyo ni pamoja na Magari madogo mawili , Malori mawili, Bajaji Saba Pikipiki kumi na kompyuta nane


Akizungumza wakati wa makabidhiano yaliyofanyika katika Ofisi za Makao Makuu ya TANESCO Manispaa ya Lindi, Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bi. Zainab Telack aliipongeza TANESCO kwa juhudi zake za kuboresha huduma ya umeme mkoani humo. Alisisitiza umuhimu wa kuvitunza vitendea kazi hivyo ili viweze kudumu kwa muda mrefu na kuwahudumia wananchi ipasavyo.

Kwa upande wake, Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi Bi. Zuwena Omary alielekeza kuwa vitendea kazi hivyo viwe chachu ya kuongeza ufanisi katika kuwahudumia wananchi pamoja na kuwafikia wale ambao bado hawajapata huduma ya umeme.

Meneja wa TANESCO Mkoa wa Lindi, Theodory Holly, alisema vifaa hivyo vitasambazwa katika maeneo yenye uhaba mkubwa wa huduma. Lengo ni kuwafikia wateja kwa urahisi zaidi na kushughulikia hitilafu za miundombinu ya umeme kwa haraka.

 

 

Simplenews subscription

The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.