SERIKALI YASAINI MKATABA UJENZI HOSPITALI YA MKOA MAHONDA

 Wizara ya Afya Zanzibar imetiliana Saini Mkataba wa Ujenzi wa Hospital ya Mkoa Mahonda na Kampuni Cross World Construction Limited.

Akizungumza baada ya Utaji Saini Mkataba huo Kaimu Waziri wa Afya Zanzibar Dkt. Saada Mkuya Salum amesema Mradi huo utakua ufumbuzi wa upatikanaji wa huduma za Kibingwa za Afya na kuipunguzia gharama Serikali ya kusafirisha Wagonjwa kutoka Nje ya Nchi.

HISTORIA YAANDIKWA MABASI YA UMEME YAWASILI ZANZIBAR

Zanzibar imeandika historia Barani Afrika baada ya kuingiza Mabasi ya Umeme kwa mara ya kwanza. Serikali kupitia mradi wa usafiri wa kisasa imepokea Mabasi Kumi ya Umeme, ikiwa ni hatua ya Mwanzo ya mpango wa kuingiza Jumla ya Mabasi Mia Moja. 

Mabasi hayo yanatarajiwa kuanza kufanya kazi rasmi Mwezi wa Tatu baada ya kukamilika kwa taratibu na Sheria husika. hatua hii inalenga kuboresha Usafiri wa Umma na kupunguza uchafuzi wa Mazingira.

TANZANIA KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA NCHI ZA NODIKI KATIKA SEKTA YA AFYA

Ubalozi wa Tanzania nchini Sweden umeratibu ushiriki wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uzinduzi wa Mkutano wa Afya kati ya nchi za Nodiki na Afrika uliofanyika tarehe 22 Januari, 2026, jijini Stockholm, Sweden, ili kujadiliana masuala ya afya ya uzazi na mtoto na mapambano dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza.
 

BULGARIA AIR YAANZA RASMI SAFARI ZAKE ZANZIBAR

Mapokezi ya Shirika la Ndege la Bulgaria Air (Bul Air) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume (AAKIA)  Alhamis ya Tarehe 22 Januari 2026

Ndege Aina ya Airbus a 320 iliwasili Uwanjani hapo Majira ya saa 5:30 Asubuhi ikitokea Jijini Sofia ikiwa na Jumla ya Abiria 180.

Shirika hilo la Ndege sasa limeanza rasmi safari zake na linatarajiwa kuwasili Zanzibar MaraTatu kwa Mwezi.

WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU NCHEMBA AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA KUSUKUMA NA KUHIFADHI MAJI MWANZA

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, ameweka jiwe la msingi la Mradi wa Ujenzi wa Miundombinu ya Kusukuma na Kuhifadhi Maji katika mkoa wa Mwanza, mradi unaolenga kuboresha usambazaji wa maji safi na salama kwa wananchi.

ZANZIBAR YAJITANGAZA KIUTALII LONDON

 Kwa mara ya kwanza katika historia ya Zanzibar imezindua Matangazo ya Utalii katika Jiji la London Nchini Uingereza kwa kubandika Matangazo yanayosomeka Tembelea Zanzibar kwenye Mabasi maarufu ya Abiria yanayoitwa London Buses.    Hatimaye historia imeandikwa.

 Mabango makubwa yanayochagiza, kushajihisha na kuuvutia Utalii wa Zanzibar yameanza kuonekana Leo kwenye Mabasi ya Abira maarufu kama London Luses Nchini Uingereza.

WANASWA KWA KUHUJUMU MRADI WA MAJI WA MIJI 28

WATU wanne wamekamatwa na Jeshi la Polisi Mkoani Tabora kwa tuhuma za kuhujumu Mradi wa Maji wa Miji 28 unaoendelea kutekelezwa na serikali katika Wilaya za Sikonge, Urambo na Kaliua ili kumaliza kero ya wananchi.

Kaimu Kamanda wa Polisi ACP Constatine Mbogambi amethibitisha kukamatwa watuhumiwa hao wakiwa na vifaa mbalimbali vilivyoibiwa kwenye mradi huo Wilayani Urambo. Akitaja baadhi ya vifaa vilivyokamatwa kuwa ni mashine kubwa 3 za kuchomelea mabomba, grenda mashine 2 za kukatia mabomba, nyaya 9 za kuunganishia grenda hizo na lita 40 za mafuta ya mitambo ya hydroliki.

WATENDAJI KITUO CHA UOKOZI MWANZA WATAKIWA KUTOA HUDUMA ZA DHARURA KWA SAA 24

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, ametoa maagizo kwa watendaji wa Kituo cha Kuratibu. Utafutaji na Uokozi cha Kikanda – Mwanza, chenye thamani ya takribani shilingi bilioni 19.8, kuhakikisha kituo hicho kinaendeshwa kwa saa 24 na kwa ufanisi wa hali ya juu.

Amesema hayo leo Januari 23, 2026 baada ya kutembelea kituo cha Kuratibu Utafutaji na Uokozi, jijini Mwanza. Huku akisisitiza kuwa huduma za uokozi ni kazi ya kuokoa maisha, hivyo hakuna uvumilivu kwa uzembe, kuchelewesha utoaji wa huduma za msaada pindi inapohitajika.

JELA MAISHA AKITUHUMIWA KULAWITI MWANAFUNZI WA MIAKA MITANO

Mkazi mmoja wa kata ya Mkata  wilaya ya Handeni Mkoani Tanga Said Mbezi (23) amehukumiwa kifo cha maisha jela baada ya kukutwa na hatia ya kumlawiti mtoto wa miaka mitano.

Hukumu hiyo imetolewa Jumatano Januari 21,2026 na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya wilaya ya Pangani  Fransisca Magwiza baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa  mahakamani hapo.

Awali ilielezwa mahakamani hapo kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo mnamo Oktoba 15,2024 katika kijiji cha Mkwaja wilaya ya Pangani kwa kumlawiti kijana wa miaka mitano ambae ni mwanafunzi wa darasa la awali.

SERIKALI INAENDELEA KUWEKEZA KWENYE MIUNDOMBINU YA SEKTA YA ELIMU

Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali inaendelea kuwekeza kwenye miundombinu ya sekta ya elimu ili kuwawezesha vijana kusoma fani tofauti ndani ya Nchi.

 Rais wa Zanzibar ameyasema hayo katika mahafali ya 19 ya Chuo kikuu cha Taifa cha Zanzibar SUZA na kuwatunuku vyeti, stashahada, shahada, shahada za uzamili na uzamivu kwa wahitimu wa Chuo hicho kwa mwaka wa masomo 2022/2023, huko Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja.

Subscribe to news
 

Simplenews subscription

The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.