DKT. MWINYI ATEMBELEA MJI WA AFCON FUMBA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameutembelea mradi wa Mji wa Afcon Fumba uliopo Mkoa wa Mjini Magharibi.

Katika Ziara hiyo Dkt. Mwinyi amembatana na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Riziki Pembe Juma, pamoja na Wadau wa Mradi wa Afcon Fumba Zanzibar.

UUNGANISHAJI UMEME MOROGORO MBIONI KUANZA, REA YAKABIDHI ENEO

Wakandarasi wanaotekelza miradi ya kusambaza umeme nchini wametakiwa kushirikiana kwa karibu na Viongozi wa Serikali za Mitaa ili utekelezaji wa miradi ya kupeleka umeme kwa wananchi iweze kuleta tija na kuchochea uchumi wa Nchi.

DKT MWINYI AWAAPISHA WAKUU WA WILAYA WAPYA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi amewaapisha Wakuu wapya wa Wilaya Watano aliowateua hivi karibuni Ikulu Zanzibar ili kuimarisha Uongozi na uwajibikaji katika utekelezaji wa Sera na mipango ya Serikali 

Zikiwa zimepita Siku Mbili tangu Uteuzi huo kutangazwa, mapema leo Viongozi hao wapya wamekula kiapo cha uaminifu, wakiahidi kuitumikia Nchi kwa weledi, uadilifu na kuzingatia sheria na taratibu za Nchi.

TANESCO YAJIPANGA KUHUDUMIA VITONGOJI 400, HANANG

Shirika la umeme Tanzania (Tanesco) Wilayani Hanang Mkoani Mnayara limejipanga  kuboresha huduma za matengenezo na maboresho ya huduma za umeme katika vitongoji zaidi ya 400 baada ya kupatiwa gari la mtambo linalotoa huduma mbali mbali ikiwemo kubadilisha nguzo na mashine umba maarufu kama transfoma.


 

SERIKALI SMT YAAGIZA KUPEWA MATIBABU BURE KIJANA MARTIN JOSEPH

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga  kwa niaba ya Mhe.Waziri Mkuu dkt.Mwigulu Nchemba  amekabidhi kiti mwendo  kwa kijana mwenye ulemavu Martin Joseph mkazi wa Babati,baada ya familia ya kijana huyo kuomba msaada kwa waziri mkuu alipokuwa kwenye ziara yake mwezi  machi /2026 mkoani humo.

REA YAWASHA UMEME VITONGOJI 307 NAMTUMBO

Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA), imewekeza jumla ya shilingi bilioni 12.1 katika miradi ya kupeleka umeme kwenye vitongoji katika wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma.

Hayo yamezungumzwa na Mbunge wa Jimbo la Namtumbo ambaye pia ni Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Juma Homera mara baada ya kuwasha umeme rasmi katika kitongoji cha Ujamaa na Kisutu vilivyopo wilaya ya Namtumbo mkoani humo.

SERIKALI ITAENDELEA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA MAWAKILI

Rais Wa Zanzibar Na Mwenyekiti Wa Baraza La Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Amekihakikishia Chama Cha Mawakili Zanzibar Kuwa Serikali Inathamini Na Kuunga Mkono Kazi Nzuri Inayofanywa Na Chama Hicho Ya Kuwasaidia Wananchi Katika Masuala Ya Kisheria.

Rais Dkt. Mwinyi Ameyasema Hayo Alipokutana Na Uongozi Wa Chama Cha Mawakili Zanzibar Ulioongozwa Na Rais Wa Chama Hicho, Wakili Joseph Shaban Magazi, Waliofika Ikulu, Zanzibar.

WAZIRI MASOUD AWAONYA WATENDAJI WA ZASCO

Waziri Wa Uchumi Wa Blue Na Uvuvi Zanzibar Mhe. Masoud Ali Mohammed Amewataka Watendaji Wa Kampuni Ya Mwani (Zasco) Kuhakikisha Mipango Waliojiwekea Inakwenda Sambamba Na Malengo Ya Serikali Ya Kuliimarisha Zao Mwani Pamoja Na Kuinua Maslahi Ya Wazalishaji Wa Hilo.

Akizungumza Na Wafanyakazi Wa Zasco Huko Mlandege Mhe. Masoud Amesema Ili Mpango Hupo Uiende Sambamba Na Malengo Ya Serikali Ni Lazima Kuwe Na   Juhudi Za Utekelezaji Kwa Watendaji Wake. 

 

ONGEZEKO LA ABIRIA UWANJA WA NDEGE WA 'AAKIA' LAAKISI MAENDELEO YA SERIKALI

Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar (ZAA) kupitia Uwanja wake wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume (AAKIA) umeendelea kushuhudia ongezeko la idadi ya abiria pamoja na miruko ya ndege, huku hatua madhubuti za kuimarisha usalama wa anga zikiendelea kupewa kipaumbele.

DKT.MWINYI AZINDUA MBIO ZA MWENGE WA UHURU PEMBA

Rais Wa Zanzibar Na Mwenyekiti Wa Baraza La Mapinduzi Dk Hussein Ali Hassan Mwinyi,Amesema Serikali Za Jamuhuri Ya Muungano Wa Tanzania Na Ya Mapinduzi Ya Zanzibar Zitaendelea Na Mapambano Dhidi Ya Ugonjwa Wa Ukimwi.

Akizindua Mbio Za Mwenge Wa Uhuru Kitaifa Huko Pemba Katika Uwanja Wa Gombani,Amesema Hivi Sasa Idadi Ya Waathirika Wa Maradhi Hayo Imepungua Kutokana Na Jitihada Zinazochukuliwa Na Serikali Zote Mbili. 

Subscribe to news
 

Simplenews subscription

The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.