TANESCO YAJIPANGA KUHUDUMIA VITONGOJI 400, HANANG

Shirika la umeme Tanzania (Tanesco) Wilayani Hanang Mkoani Mnayara
English

Shirika la umeme Tanzania (Tanesco) Wilayani Hanang Mkoani Mnayara limejipanga  kuboresha huduma za matengenezo na maboresho ya huduma za umeme katika vitongoji zaidi ya 400 baada ya kupatiwa gari la mtambo linalotoa huduma mbali mbali ikiwemo kubadilisha nguzo na mashine umba maarufu kama transfoma.


 

Gari hilo  maalumu la mtambo  limezinduliwa na  mkuu wa Wilaya ya Hanang Halmishi Hazali  nakusema kuwa ujio wa gari hilo litasaidi katika utendaji kazi na  kutatatua  changamoto mbalimbali zinazo sababisha kukatika kwa umeme katika wilaya hiyo hasa katika kipindi hiki cha mvua.

Image removed.

Meneja wa Tanesco Wilaya ya Hanang amesema ujio wa gari hilo utaongeza kasi ya uboreshaji wa huduma za umeme katika vitongoji 400 katika wilaya hiyo na kuwaondolea hadha wananchi ya kukoseka kwa umeme pindi inapotokea kuungua kwa mashine umba maarufu kama transfoma.


 

kwa upande wake mbunge wa jimbo la Hanang Asia Halamga amepongeza juhudi za serikali katika kuhudumia wananchi wa jimbo hilo kwenye mambo mbalimbali ya maendeleo ikiwemo umeme ,maji pamoja na Barabara.

 

Simplenews subscription

The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.