DKT.MWINYI AZINDUA MBIO ZA MWENGE WA UHURU PEMBA

DKT.MWINYI
English

Rais Wa Zanzibar Na Mwenyekiti Wa Baraza La Mapinduzi Dk Hussein Ali Hassan Mwinyi,Amesema Serikali Za Jamuhuri Ya Muungano Wa Tanzania Na Ya Mapinduzi Ya Zanzibar Zitaendelea Na Mapambano Dhidi Ya Ugonjwa Wa Ukimwi.

Akizindua Mbio Za Mwenge Wa Uhuru Kitaifa Huko Pemba Katika Uwanja Wa Gombani,Amesema Hivi Sasa Idadi Ya Waathirika Wa Maradhi Hayo Imepungua Kutokana Na Jitihada Zinazochukuliwa Na Serikali Zote Mbili. 

Katika Uzinduzi Huo Dkt. Mwinyi Amemkabidhi Mwenge Wa Uhuru Mkuu Wa Mkoa Wa Kusini Pemba, Rashid Hadidi Rashid Kwa Kuanza Kwa Mbio Zake Katika Mkoa Huo Na Kuzindua Miradi Mbalimbali Ya Maendeleo Ambayo Inalenga Kuwanufaisha Wananchi Kiuchumi Na Kijamii

“Kaulimbiu Ya Mwenge Wa Uhuru Kwa Mwaka Huu Ni Tanzania Yetu Tushirikiane Kwa Pamoja Kuleta Maendeleo.”

 

Simplenews subscription

The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.