WANANCHI WAOMBA KASI YA MAPAMBANO DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA IONGEZEKE

DAWA ZA KULEVYAS
English

Wananchi wa Kijiji cha Kaole Ufundi ,Bagamoyo Mkoani Pwani wameiomba Serikali kuongeza nguvu katika mapambano dhidi ya biashara haramu ya Dawa za kulevya ili kukomesha biashara hiyo katika Jamii.

Wananchi hao wametoa kauli hiyo wakati Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Nchini DCEA ikikamata virobo 18 vyenye vifurushi 1062 vya dawa za kulevya aina ya Mirungi, Boti ya Mwendokasi pamoja na watuhumiwa Wanne waliokuwa wanasafiri na chombo hicho katika ufukwe wa Magambani Kaole Ufundi, Bagamoyo Mkoa Pwani.

Akizungumza na Waandishi wa Habari katika Eneo la tukio Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupamabana na Dawa za Kulevya Aretas Lyimo anasema dawa hizo haramu pamoja na Watuhumiwa hao wamekatwa katika Operesheni maalum iliyofanyika Usiku wa Kuamkia April 14 Mwaka huu.

Aidha Kamishna Lyimo amesema Boti hiyo imekuwa ikisafirisha Dawa za Kulevya kwa muda mrefu hivyo kukamatwa kwake inapunguza mzunguko wa kusafirisha Dawa hizo haramu.

 

Simplenews subscription

The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.