Michezo

REAL MADRID YATWAA UBINGWA WA LALIGA 2023/2024

    Real Madrid imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Uhispania (LaLiga) ikiwa imesaliwa na michezo minne mkononi baada ya kushinda magoli 3-0 dhidi ya Cadiz.

   Baada ya Madrid kutangazwa mabingwa wa La Liga nafasi ya pili inashikwa na Girona FC yenye alama 74 huku nafasi ya tatu ikishikwa na Barcelona yenye alama 73, timu zote zikiwa zimecheza michezo 34.

 

SERIKALI KUJENGA VITUO VYA MICHEZO UNGUJA NA PEMBA

     Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe.Tabia Maulid Mwita amesema Serikali ina mpango wa kuimarisha miundo mbinu ya Michezo kwa kujenga Vituo vya Michezo Academy kwa kila Mkoa Unguja na Pemba.

    Waziri Tabia ametoa kauli hiyo, wakati akiwaaga Wachezaji na Viongozi wa Timu ya Wasichana ya Zanzibar Spark, inayotarajia kushindana katika Mshindano ya Mpira wa Miguu ya Kimataifa Nchini Ufaransa.

DKT.NDUMBARO AKUTANA NA VIONGOZI WA CHAMUSTA

     WAZIRI wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Chama cha Maafisa Utamaduni na Sanaa Tanzania (CHAMUSTA) na kujadili masuala mbalimbali ikiwemo suala la kukabiliana na mmomonyoko wa maadili katika jamii, uboreshaji wa mazingira ya utendaji kazi ya maafisa utamaduni pamoja na ubidhaishaji wa urithi wa utamaduni kwa ajili ya utalii wa utamaduni, Malikale na michezo.

WADHAMINI WAMEOMBWA KUENDELEA KUWASAIDIA WANAMICHEZO

Viongozi na Wanamichezo mbali mbali wameshauriwa kuendelea kuweka jitihada kwenye kukuza Michezo kwa kuzisaidia Timu ili ziweze kujikwamua Kiuchumi.

Ushauri huo umetolewa na Meneja wa Taasisi Afrocare Phamasi, Grace Edgar wakati wakikabidhi vifaa vya Michezo kwa Timu ya Jamhuri FC,   amesema kudhamini wao utahakikisha Vijana Wanacheza Mpira wakiwa na Afya njema ili kuweza kufanya vizuri katika Michezo yao

Kocha Mkuu wa Timu hiyo, Ramadhani Abrahman Madundo amesema kukosekana kwa  udhamini kulichangia Timu yake kutokufanya vizuri kwenye Mashindano.

KATIBU BARAZA LA MICHEZO AKUTANA NA UONGOZI WA TAASIS YA 'ZYBA'

       Katibu Mtendaji Baraza la Michezo Zanzibar, Said Kassim amekutana na Mkurugenzi wa Taasisi ya Zanzibar Youth Basketball (ZYBA) Abdul Azizi Salim na kutoa Baraka za Mashindano ya ZYBA BASKETBALL 2024, yatakayoanza hivi karibuni.

     Viongozi wa Baraza wameipongeza ZYBA kwa kuweza kuandaa jambo kubwa na zuri lakini pia litakaloweza kuitangaza Zanzibar Kimichezo.

TANZANIA YAINGIA MAKUBALIANO NA IVORY COAST KATIKA SEKTA YA MICHEZO

     Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imeingia makubaliano ya ushirikiano na Wizara ya Michezo ya Ivory coast  katika masuala mbalimbali ya uendelezaji wa Sekta ya michezo.a                   

MPIRA WA MIGUU UNAENDESHWA KWA SHERIA NA KANUNI NA SIO MIHEMKO

     Rais wa shirikisho la mpira wa Miguu Zanzibar, Suleiman Mahmoud Jabir amesema kuwa “Mpira wa miguu unaendeshwa kwa sheria na kanuni zake sio kwa mihemko ya baadhi ya watu”

    Rais wa ZFF ameyasema hayo wakati akifungua mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Mpira wa Miguu wilaya ya Magharibi B katika Skuli ya Samia Suluhu Hassan iliyopo Mwanakwerekwe.

     Amesema Mkutano Mkuu ndiyo chombo muhimu katika kupanga mambo mbali mbali ya Wilaya husika pamoja na mipango ya uendeshaji wa Mpira kwa wilaya husika.

VIJANA 49 WAPATIKANA KWENYE KUSAKA VIPAJI

Katibu Mkuu Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF) Hussein Ahmada amesema jumla ya Vijana 49 wamepata fursa ya

kuchaguliwa kwenye zoezi maalum la kusaka Vipaji vya Vijana

Wadogo.

Hussein Ahmada amesema chini ya Umri wa Miaka 15 wamepatikana Vijana 22 na chini ya umri wa Miaka 17 wamepatikana Vijana 27 katika zoezi hilo.

Hussein amewaomba Wazazi kuwaunga Mkono Vijana wao katika kufanikisha mafanikio ya Mpira wa Miguu Zanzibar.

Zoezi hilo la kusaka Vipaji vya Wachezaji Vijana imeandaliwa

SIMBA NA YANGA KIBARUA KIZITO LEO

   Meneja Habari na Mawasilino wa Klabu ya Simba Ahmed Ali amesema Kikosi chao kiko vyema kuwakabili Al-ahly ya Misri licha ya kupoteza Mchezo wao wa Awali.

    Ahmed amesema wamefanya Mazoezi yao ya Mwisho kuelekea Mchezo huo na hawana wasi wasi juu ya kupindua meza na kutinga Nusu Fainali.

    Aidha Ahmed amesema haitakuwa rahisi kupata Matokeo lakini wamejipanga vyema na wako tayari kupambana.

TFF YAANZA MIKAKATI YA KUIBUA VIPAJI

   Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeanza mkakati wa kuibua Vipaji vya Mpira wa Miguu kwa kuzipatia Mipira Mia Mbili Arobaini Shule za Msingi Sita za Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro 

    Akikabidhi Mipira hiyo kwa Walimu wa Shule hizo za Msingi Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Morogoro (MRFA) Paschal Kihanga amesema lengo la TFF na Serikali ni kuhakikisha wanatengeneza Vipaji vya Mpira kuanzia Watoto Wadogo.

Subscribe to Michezo
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.