SHILINGI TRILIONI 2.72 KUIMARISHA MAWASILIANO YA SIMU

PROF.MAKAME MBARAWA

Kuimarika kwa Mawasiliano katika Ziwa Victoria, Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limeandaa hati ya makubaliano na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) pamoja na Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) kwa ajili ya Ujenzi wa Minara Mitatu ya Mawasiliano ya Simu. 

Hayo yameelezwa Bungeni Jijini Dodoma na Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na Matumizi ya Wizara yake kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 ambapo ameliomba Bunge kuidhinishiwa ujumla ya  Trilioni 2.72.

Aidha Prof. Mbarawa amesema kuwa Serikali imeendelea kushirikisha  sekta Binafsi katika uendeshaji wa Bandari ya  Dar es salaam kwa baadhi ya maeneo ya  Bandari kwa kuingia Ubia na Kampuni Binafsi  katika kuendeleza na kuendesha shughuli za  Bandari kuanzia Gati na. 4 hadi 7. 

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.