MPIRA WA MIGUU UNAENDESHWA KWA SHERIA NA KANUNI NA SIO MIHEMKO

Rais ZFF

     Rais wa shirikisho la mpira wa Miguu Zanzibar, Suleiman Mahmoud Jabir amesema kuwa “Mpira wa miguu unaendeshwa kwa sheria na kanuni zake sio kwa mihemko ya baadhi ya watu”

    Rais wa ZFF ameyasema hayo wakati akifungua mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Mpira wa Miguu wilaya ya Magharibi B katika Skuli ya Samia Suluhu Hassan iliyopo Mwanakwerekwe.

     Amesema Mkutano Mkuu ndiyo chombo muhimu katika kupanga mambo mbali mbali ya Wilaya husika pamoja na mipango ya uendeshaji wa Mpira kwa wilaya husika.

      Aidha, wakati umefika kwa Chama hicho kuanza kutangaza bidhaa zao ili kupata ufadhili katika Mashirika mbali mbali hapa Zanzibar na Tanzania bara kwa ujumla

     Nae Mrajisi wa Vyama vya Michezo Zanzibar, Aboubakar Mohammed Lunda amesema “Wajumbe wana wajibu wa kufanya Mikutano yao Mikuu katika Vilabu vyao sio tu kwa upande wa Chama husika na kama watafanya hivyo sio sahihi kwa Vilabu.

    Mapema Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu, Wilaya ya Magharibi 'B', Ndg. Maulid  Abdallah ,amesema kuwa “Mkutano huo Mkuu wa Mwaka lengo lake ni kuona Wajumbe wa Vilabu wanatoa maoni yao katika kuwendesha mpira ndani ya Wilaya hiyo.

 

Tags
hot
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.