MALINDI YAANZA KWA KISHINDO

Naibu Waziri Wa Wizara Ya Habari, Sanaa, Utamaduni Na Michezo Ali Abdul-Ghulam Hussein Amesema Serikali Itaendelea Kuwekeza Kwa Katika Sekta Ya Michezo Kwa Kujenga Na Kuimarisha Miundombinu Ya Viwanja Vya Michezo Ili Kuendeleza Vipaji Vya Vijana Nchini.

MICHEZO NI FURSA ZA AJIRA KWA VIJANA

Mbunge Wa Jimbo La Donge Sadifa Juma Khamis, Ameeleza Kuwa Uwepo Wa Viwanja Bora Vya Michezo Ni Muhimu Katika Kukuza Vipaji Sambamba Na Kutoa Fursa Za Ajira Kwa Vijana.

GAMONDI ASAINI MKATABA WA KUWA KOCHA MKUU TAIFA STARS

Serikali Ya Jamhuri Ya Mungano Wa Tanzania Imempa Mkataba Wa Miaka Miwili Kaimu Kocha Mkuu Wa Taifa Stars Miguel Gamondi
 Na Sasa Kuwa Kocha Mkuu Ajili Ya Kuifundisha Timu Hiyo Ikiwa Ni Miongoni Mwa Mikakati Ya Kufanya Vizuri Katika Mashindano
 YaAfcon 2027

MLANDEGE WAVUNA ALAMA 3 DHIDI YA POLISI PBZ PL

Mabingwa Watetezi Wa Ligi Kuu Soka Zanzibar Mlandege Fc Imeibuka Kidedea Baada Ya Ushindi Wa Magoli Mawili Kwa Moja Baada Dhidi Ya Polisi Zanzibar Mchezo Uliochezwa Jioni Ya Leo Katika Uwanja Wa Mao

MO, DEWJI AMHOJI MANGUNGU MTANDAONI KUHUSU MABADILIKO YA KLABU YA SIMBA

Mwekezaji wa klabu ya Simba na Mfanyabiashara Mohammed Dewij ameibuka Mtandao na kuhoji hatua iliyofikiwa katika mchakato wa Mabadiliko ya Mfumo wa uendeshaji wa Klabu ya Simba.

Swali hilo limeibuka wakati Uongozi wa klabu ukitangaza rasmi kurejesha usajili wa wanachama kwenye mkutano wake na Vyombo vya Habari Jijini Dar es Salaam. Leo Februari 10,2026.

JKU SC YAUPIGIA HESABU UBINGWA WA LIGI KUU ZNZ

Katibu Wa Klabu Ya Jku Sc Khatibu Shazil Khatibu Amesema Timu Yao Inaendelea Na Maandalizi Ya Kuhakikisha Mzunguko Wa Pili Wanafanya Vizuri Ili Kubeba Ubingwa

Katibu Shazil Amesema Malengo Ya Jku Ni Kufanya Vizuri Katika Michuwano Ya Ligi Kuu Na Kombe La Fa Huku Akigusia Kuhusu Usajili Waliofanya.

DKT. MWINYI AFUNGUA VIWANJA VYA MATUMBAKU SPORTS COMPLEX

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Serikali itaendelea kujenga  miundombinu ya  viwanja vya michezo ili kuwawezesha vijana kujiajiri kupitia michezo.

Akifungua viwanja vipya vya Matumbaku Sports Complex vinavyo jumuisha michezo mbali mbali ikiwemo mpira wa wavu ,kikapu, mpira wa Pete na mpira miguu, Dkt. Mwinyi amesema Kutokana na ukuaji wa soko la Ajira Duniani kupitia michezo, Serikali imeona ipo haja ya kuimarishwa viwanja hivyo ili kukuza utalii na kuimarisha uchumi wa nchi.

CARLO ANCELOTTI BADO YUPO SANA REAL MADRID HADI 2026

Meneja wa Real Madrid, Carlo Ancelotti ametia saini mkataba mpya na klabu hiyo utakaodumu hadi Juni 2026.

Muitaliano huyo, mwenye umri wa miaka 64, aliteuliwa Bernabeu kwa mara ya pili mwaka 2021 kwa mkataba wa awali wa miaka mitatu.

 

Alihusishwa na kuchukua nafasi ya meneja wa Brazil mapema mwaka huu lakini akasema anataka kubaki katika klabu hiyo.

 

Ancelotti ameshinda mataji 10 kama kocha wa Real, yakiwemo mawili ya Ligi ya Mabingwa - hivi karibuni katika msimu wake wa kwanza akiwa na klabu hiyo mnamo 2021-22.

 

EMMA KUREJEA TENA KUCHEZA TENNIS BAADA YA UPASUAJI WA MIKONO

Mwingereza Emma Raducanu anasema anahisi kuzaliwa upya wakati huu, akijiandaa kurejea tena kwenye tenisi huko Auckland baada ya miezi minane nje ya uwanja.

Bingwa wa US Open 2021 alicheza mechi tisa pekee mnamo 2023, akiwa nje ya uwanja tangu Aprili.

Raducanu, mwenye umri wa miaka 21, alifanyiwa upasuaji wa mikono yote miwili na kifundo cha mguu wake wa kushoto mwezi Mei, na ameshuka hadi nafasi ya 298 katika viwango vya ubora duniani.

AKRAM NI NYOTA WA KWANZA KUFUNGA BAO UWANJA WA NEW AMAAN COMPLEX.

Nyota wa klabu ya KVZ, Akram Mhina Omar ndie mchezaji wa kwanza kufunga bao katika Uwanja wa New Amaan Complex, baada ya matengenezo makubwa yaliyochukua takribani miezi Sita, katika mchezo wa michuano ya Mapinduzi Cup dhidi ya Jamhuri.

New Amaan Compex, ulifunguliwa rasmi Disemba 27, 2023 saa kumi na moja dakika 23 jioni, na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi baada ya ukarabati huo kupita.

Subscribe to sports
 

Simplenews subscription

The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.