AKRAM NI NYOTA WA KWANZA KUFUNGA BAO UWANJA WA NEW AMAAN COMPLEX.
Nyota wa klabu ya KVZ, Akram Mhina Omar ndie mchezaji wa kwanza kufunga bao katika Uwanja wa New Amaan Complex, baada ya matengenezo makubwa yaliyochukua takribani miezi Sita, katika mchezo wa michuano ya Mapinduzi Cup dhidi ya Jamhuri.
New Amaan Compex, ulifunguliwa rasmi Disemba 27, 2023 saa kumi na moja dakika 23 jioni, na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi baada ya ukarabati huo kupita.








