Rais Wa Zanzibar Na Mwenyekiti Wa Baraza La Mapinduzi Dkt, Hussein Ali
Mwinyi Amewasisitiza Viongozi Wakuu Katika Taasisi Za Umma Kuzingatia Upendo,Uadilifu Na Haki Katika Kuwasimamia Wanaowaongoza Na Utekelezaji Wa Majukumu Yao.
Akizungumza Katika Kongamano La Tatu La Kiimani Kwa Viongozi Wa Serikali Lililoandaliwa Na Afisi Ya Mufti Mkuu Wa Zanzibar, Ameeleza Kuwa Kongamano Hilo Ni Msingi Wa Kukumbushana Umuhimu Wa Kuzingatia Maadili Katika Utumishi Wa Umma Na Jukwaa Muhimu La Kujifunza Uwiano Wa Kazi Kwa Misingi Ya Kiimani