Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi ameipongeza Hospitali ya Benjamin Mkapa kwa mageuzi namafanikio makubwa ya utoaji wa huduma za matibabu ya kibingwa kwa Wananchi.
Akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo Prof. Abel Makubi akiambatana na ujumbe wake waliofika Ikulu Zanzibar DÄ·t.Mwinyi amesifia huduma hizo ikiwemo matibabu ya Figo ,Moyo na Ubongo kufanyika hapa Nchini ,hatua aliyopunguzia Serikali na Wananchi gharama za kuwapeleka Wagonjwa Nje ya Nchi.