KATIBU NEC ATEMBELEA MIRADI YA AFYA HOSPITALI YA RUFAA KILIMANJARO
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) wa Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI), Rabia Abdalah, ambaye pia ni mlezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoani Kilimanjaro, ametembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro kwa lengo la kujionea utekelezaji wa baadhi ya miradi ya maendeleo inayoendelea katika hospitali hiyo.
