Chama cha ACT Wazalendo Zanzibar kimeiomba Tume ya Uchaguzi Zanzibar–ZEC kusimamisha zoezi la uteketezaji wa nyaraka na vifaa vya Uchaguzi kwa kile walichodai ni mpaka mashauri yaliyoko Mahakamani yamalizike.
Kauli hii imekuja kutokana na Tamko la Tume ya Uchaguzi lililotolewa hapo Jana likieleza nia ya Tume kuteketeza nyaraka zote za Uchaguzi wa Mwaka 2025 kwa baada ya Siku 90 kwa mujibu wa Sheria.
Ni Siku Moja tu imepita toka Mkuu wa Kurugenzi ya huduma za sheria wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Ndg.Maulid Mohamed kutangaza nia ya Tume kutekeza nyaraka zote za Uchaguzi wa Mwaka 2025 kwa mujibu wa Sheria.
Hii leo Makamu Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Zanzibar Ndg.Ismail Jussa amekutana na Vyombo vya Habari akiitaa Tume iwe na subira ya kutekeleza zoezi hilo kwa lengo la kutenda haki.
Hata hivyo Tume ya Uchaguzi imetoa imejitokeza kwa Mara ya Pili kutoa ufafanuzi kuhusu hatua hii ya uteketezaji wa nyaraka za Uchaguzi Mkuu kwa mujibu wa Sheria. Jaji George Kazi ni Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar.


