MAONESHO YA KITAIFA YA WAKANDARASI YAZINDULIWA GEITA

MAONESHO
English


Zaidi ya makampuni 60 kutoka ndani na nje ya nchi yanashiriki katika Maonesho ya Wakandarasi, Wahandisi, Sekta ya Viwanda, na Watengenezaji wa Mitambo ya Uchimbaji Madini yaliyozinduliwa rasmi leo mkoani Geita.

Maonesho hayo yanayofanyika katika Viwanja vya Samia Suluhu Hassan (Bombambili), Manispaa ya Geita, yanalenga kutoa elimu kwa jamii na wadau wa sekta hizo kuhusu mbinu za kisasa na utaalamu wa uendeshaji wa miradi ya ukandarasi na uchimbaji madini.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mratibu wa Maonesho, Injinia Bernard Mwata, amesema kuwa tukio hilo limevuta hisia za washiriki wa kimataifa na mashirika mbalimbali ya hapa nchini, jambo linaloashiria kukua kwa sekta ya ujenzi na madini nchini Tanzania.

Kwa upande wake, Afisa kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara, Anneth Ngowi, amesisitiza utayari wa Wizara hiyo katika kushirikiana na kampuni za umma na binafsi ili kukuza uchumi wa viwanda.

Alitoa wito kwa wakazi wa Geita na mikoa jirani kujitokeza kwa wingi ili kujionea teknolojia mpya na kujifunza kuhusu mitambo mbalimbali inayofanya kazi katika sekta hizo.

Nao baadhi ya washiriki wameipongeza kampuni ya MAT Builders and Contractors Global Expo kwa uratibu makini wa maonesho hayo, wakibainisha kuwa ni fursa adhimu kwa wananchi kupata maarifa yatakayosaidia kuboresha shughuli zao za kila siku.

 

Simplenews subscription

The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.