ACT WAZALENDO YAIOMBA ZEC KUSIMAMISHA UCHOMAJI NYARAKA ZA UCHAGUZI
Chama cha ACT Wazalendo Zanzibar kimeiomba Tume ya Uchaguzi Zanzibar–ZEC kusimamisha zoezi la uteketezaji wa nyaraka na vifaa vya Uchaguzi kwa kile walichodai ni mpaka mashauri yaliyoko Mahakamani yamalizike.
Kauli hii imekuja kutokana na Tamko la Tume ya Uchaguzi lililotolewa hapo Jana likieleza nia ya Tume kuteketeza nyaraka zote za Uchaguzi wa Mwaka 2025 kwa baada ya Siku 90 kwa mujibu wa Sheria.
