KATIBU NEC ATEMBELEA MIRADI YA AFYA HOSPITALI YA RUFAA KILIMANJARO

CCM
English

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) wa Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI), Rabia Abdalah, ambaye pia ni mlezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoani Kilimanjaro, ametembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro kwa lengo la kujionea utekelezaji wa baadhi ya miradi ya maendeleo inayoendelea katika hospitali hiyo.

Katika ziara hiyo, Rabia alipata fursa ya kukagua miundombinu pamoja na huduma mbalimbali zinazotolewa kwa Wananchi, huku akielezwa hatua zilizofikiwa katika Miradi hiyo na namna inavyolenga kuboresha upatikanaji wa huduma bora za Afya kwa wakazi wa Mkoa huo na Maeneo jirani.

Amesisitiza umuhimu wa kuendelea kusimamia kikamilifu utekelezaji wa Miradi hiyo ili kuhakikisha inakamilika kwa wakati na kuwanufaisha Wananchi kama ilivyokusudiwa. 

 

Simplenews subscription

The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.