RAIS DKT. MWINYI AKIRI KUWA WANAWAKE WALIKUWA NA MCHANGO MKUBWA KATIKA KUFANIKISHA KUFANYIKA KWA MUUNGANO

Dkt Mwinyi kwenye mdahalo

       Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi , Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Wanawake walikuwa na mchango mkubwa kufanikisha kufanyika kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa kuzingatia tulipotoka, tulipo na tunakolekea katika harakati za historia ya nchi yetu .

      Rais Dk.Mwinyi amesema hayo katika Mdahalo wa kutathimini Nafasi ya Mwanamke wa Tanzania katika Miaka 60 ya Muungano wa Tanzania ulioandaliwa na Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam tarehe 25 Aprili 2024.

     Aidha Rais ameipongeza UWT kwa kuendelea kuwa kinara katika kubuni na kutekeleza mambo mbalimbali yenye lengo la kukiimarisha Chama Cha Mapinduzi na kukiunganisha Chama na wananchi.

       Rais Dk.Mwinyi amesema Muungano wa Tanzania umeleta faida nyingi za kiuchumi, kisiasa na kijamii kwa wananchi wa pande zote mbili za Muungano.

      Halikadhalika Rais Dk.Mwinyi ameeleza kuwa dhamira njema ya Waasisi wa Taifa letu ya kuunganisha nchi zetu mbili imeendelezwa na Viongozi wa pande zote mbili za Muungano kwa kuudumisha, kuimarisha kwa kuzipatia ufumbuzi changamoto zilizojitokeza hadi sasa na hivyo kuufanya uwe imara zaidi.

     Kwa upande mwingine Rais Dk.Mwinyi amewahimiza wanachama wa CCM kujiandaa vya kutosha ushiriki wao katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa upande wa Tanzania Bara mwaka huu na Uchaguzi mkuu mwakani 2025 katika pande zote mbili za Jamhuri ya Muungano

    Vilevile pia amehamasisha Wanawake kushiriki kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali wakati wa chaguzi zitakapofikia.

 

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.