TAPHATA WAFATILIA UPANUZI WIGO WA AJIRA KWA WATEKNOLOJIA DAWA

Akizungumza katika mahojiano maalum Bw Milandu
English

Rais wa Chama cha Wateknolojia Dawa Tanzania(TAPHATA) Bw.Thabiti Milandu amesema uongozi wa chama hicho unaendelea kufanya jitihada za dhati na juhudi za makusudi katika kuhakikisha unafuatilia utanuzi na upanuzi wa wigo wa ajira nchini ambapo taaluma hiyo inazalisha watu wengi na uhitaji ni mkubwa.

Akizungumza katika mahojiano maalum Bw Milandu ameweka bayana kuwa kufuatia ongezeko la mapinduzi ya viwanda vya dawa hapa nchini nafasi hiyo itasaidia katika kuongeza idadi kubwa ya ajira kwa wateknolojia dawa.

Ameongeza kuwa uwepo viwanda hivyo vitasaidia kuanzishwa kwa huduma ya uchanganyaji dawa ndani ya kituo na uzalishaji wa baadhi ya bidhaa za afya ndani ya kituo ikiwemo Spirit,Sabuni,pamoja na Vitakasa mikono.

Hivyo ametumia nafasi hiyo kuwakumbusha wanataaluma ambao hawajajiunga na chama hicho kujiunga na kuhakikisha wanafanya mitihani ya leseni kwani ndio kigezo pekee cha kujiunga na chama na kuajiriwa mahala popote nchini.

Pia amewakaribisha wanachama wa Chama cha Wateknolojia Dawa Tanzania(TAPHATA) katika mkutano mkuu wa chama unaofanyika kila mwaka ukiambatana na kauli mbiu inayobeba ujumbe mahsusi,ambapo kwa mwaka huu unatarajiwa kufanyika jijini Arusha kuanzia tarehe 27 Hadi 30 Oktoba 2026.

 

Simplenews subscription

The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.