JAPAN NA ZANZIBAR ZAAHIDI KUSHIRIKIANA

Makamu Wa Pili Wa Rais Wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla Amesema Serikali Ya Mapinduzi Ya Zanzibar Itaendeleza Uhusiano Ulipo Kati Ya Serikali Ya Japan Na Zanzibar Uliodumu Kwa Muda Mrefu.

Mhe. Hemed Ameyasema Hayo Alipofanya Mazungumzo Na Balozi Wa Japan Nchini Tanzania Yoichi Mikami Afisini Kwake Vuga Zanzibar.

Amesema Uhusiano Uliopo Kati Ya Tanzania Na Japan Utaendelea Kukuza Ushirikiano Katika Pande Zote Mbili Katika Kuimarisha Sekta Za Kilimo, Biashara, Maji Safi Na Salama, Maendeleo Ya Viwanda, Utalii Na Miundombinu Mbali Mbali.

SEKTA YA FEDHA NGUZO YA UCHUMI ENDELEVU

Waziri Wa Fedha Na Mipango Dkt. Malik Akili Amesema Sekta Ya Fedha Ni Moja Ya Eneo Litakalofanya Uchumi Wa Zanzibar Kuwa Endelevu Kama Ilivyoainishwa Katika Dira Ya Maendeleo Ya 2050.

Dkt. Malik Ameyasema Hayo Katika Ufunguzi Wa Tawi La Benki Kcb Mkunazini Zanzibar.

Katika Ufunguzi Wa Benki Hiyo, Dkt. Malik Amesema Sera Hiyo Inalenga Kuwepo Na Mageuzi Ya Kiuchumi Kwa Kuhakikisha Watu Wote Wanajumuishwa Katika Masuala Ya Kifedha Ikiwemo Huduma Za Kibenki.

MO, DEWJI AMHOJI MANGUNGU MTANDAONI KUHUSU MABADILIKO YA KLABU YA SIMBA

Mwekezaji wa klabu ya Simba na Mfanyabiashara Mohammed Dewij ameibuka Mtandao na kuhoji hatua iliyofikiwa katika mchakato wa Mabadiliko ya Mfumo wa uendeshaji wa Klabu ya Simba.

Swali hilo limeibuka wakati Uongozi wa klabu ukitangaza rasmi kurejesha usajili wa wanachama kwenye mkutano wake na Vyombo vya Habari Jijini Dar es Salaam. Leo Februari 10,2026.

NDANI YA SIKU 100 WIZARA TUMEFANIKIWA KUTOA AJIRA 2,300

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar, Dkt. Mngereza Mzee Miraji, ameeleza utekelezaji wa majukumu ya Wizara ya Afya kuanzia ngazi ya msingi hadi ngazi ya juu ya rufaa, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha mfumo wa huduma za afya Zanzibar.

Ndani ya siku 100 za utekelezaji, Wizara imefanikiwa kuajiri wahudumu wa afya ngazi ya jamii 2,300, hatua iliyopanua upatikanaji wa huduma za afya mashinani, sambamba na kuhakikisha mishahara inalipwa kwa wakati kutokana na uongozi na maelekezo ya Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi.

Subscribe to
 

Simplenews subscription

The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.