MAHAKAMA YAPENI KIPAUMBELE MASHTAKA YA UKATILI DC KAGANDA.

Serikali Mkoani Manyara
English

Serikali Mkoani Manyara imeishauri mahakama kuyapa kipaombele mashauri yanayohusu ukatili wa kijinsia na kutoa adhabu yenye kuleta majuto kwa jamii na wanaohusika na matukio hayo.


Kauli hiyo kwa mahakama Kanda ya Manyara imetolewa na Mkuu wa wilaya ya Babati Emanuela Kaganda kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga wakati akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya sheria Nchini yaliyofanyika kwenye viwanja vya mahakama hiyo Mkoani humo.


Naye jaji Mfawidhi mahakama kanda ya manyara  Ilvin Mugeta amesema   kasi  ya usikilizwaji na utoaji wa maamuzi ya kesi mbalimbali ikiwemo kesi za ukatili umeongezeka ,na kuwataka  wananchi wenye mirathi i yao mahakamani kwenda kuzichukua kabla ya mwezi March mwaka huu na kabla ya kuahamishiwa katika mfuko wa taifa kwa mujibu wa sheria.

Nao baadhi ya Wananchi waliofika kwenye maashimisho hayo,hususan waliowahi kuwa na mashauri yao mahakamani hapo wametoa maoni yao   juu ya mwenendo wa usikilizwaji na utoaji wa maamuzi katika mahakama hiyo nakusema kwa sasa hali ni nzuri na namna ya uendeshwaji wa kesi hiyo. Nae mwenyekiti wa Chama cha wanasheria Tanganyika Tadei Lista  amesema mahakama kuzingatia utoaji wa haki bila upendeleo inaleta utulivu na kuchangia maendeleo ya Taifa katika muktadha wa utafsiri wa sheria kwa usahihi.

 

Simplenews subscription

The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.