BILIONI MIA SABA ZATUMIKA KUJENGA KIWANDA CHA SUKARI KILOMBERO

KIWANDA CHA SUKARI
English

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais mipango na uwekezaji Professa Kitila Mkumbo amesema kiwanda kipya cha sukari Kilombero K4  kilichopo Mkoani Morogoro ambacho kinajengwa kwa gharama ya shilingi Billioni mia saba kinatarajiwa kuanza uzalishaji wake Mwezi Juni Mwaka huu ni moja ya Kiwanda ambacho kitafanya lengo ya kukuza uchumi kuelekea Mwaka 2050  kufikia dola trilioni moja.

Akizungumza mara baada ya kufanya Ziara ya kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Kiwanda cha Sukari Kilombero K4 Profesa Kitila Mkumbo amesema Kiwanda hicho ni kikubwa kwa Nchi za Afrika ya Mashariki na Kusini mwa Afrika.

Aidha amesema uwekezaji huo utaweza kuzalisha Sukari maradufu na kusaidia Tanzania kujitosheleza katika uhitaji wa Sukari pamoja na kuongeza ajira kwa Vijana huku Mkurugenzi Mtendaji Kiwanda cha Sukari Kilombero Guy Williams akieleza namna walivyofanya kazi mpaka kufika hatua hii pamoja na namna kitakavyowasaidia Wakulima katika uzalishaji wa Miwa.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari Profesa. Kenneth Bengesi anaeleza ndoto ya Serikali katika kuondoa changamoto ya uagizaji wa Sukari kutoka Nje ya Nchi.

 

 

Simplenews subscription

The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.