WATOTO WENYE ULEMAVU WATOA KILIO CHAO HADHARANI

WAZIRI GWAJIMA
English

Wadau wa Maendeleo, Watunga Sera, Mashirika yasiyo ya Kiserikali pamoja na asasi za kiraia kutoka Nchi 23 Duniani wamekutana Jijini Arusha katika Jukwaa la Kimataifa la kujifunza kuhusu usawa wa kijinsia, ujumuishi wa watu wenye ulemavu na ushirikishwaji wao katika Jamii.

Katika jukwaa hilo, Watoto wenye ulemavu wameeleza matatizo yanayowakabili na kuiomba Serikali kuimarisha  mazingira ya Skuli na Jamii kubadili mtazamo na kuacha unyanyapaa ili kupata haki na fursa sawa 

Akizungumza katika Mkutano huo, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Doroth Gwajima akaeleza kuwa watu wenye ulemavu wanapaswa kutazamwa kwa jicho la usawa, akisisitiza kuwa wana vipaji na mchango muhimu kwa Taifa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa World Vision Tanzania James Anditi, amesema Wadau wanapaswa kuyafanyia kazi mapungufu yaliyopo kwa kuwa maendeleo jumuishi hayawezekani bila kuwashirikisha watu wenye ulemavu.

 

Simplenews subscription

The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.