WANAOSAFIRISHA MAGENDO WATAKIWA KUCHUKULIWA HATUA

KARAFUU ZA MAGENDO
English

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mgeni Khatib Yahya ameagiza kuchukuliwa hatua kali za kisheria dhidi ya wale waliohusika kutaka kutorosha Magunia 15 ya Karafuu katika Bandari ya Wambaa Wilaya ya Mkoani

Akizungumza na Wananchi, Mkuu wa Mkoa amesema Serikali haitasita kutumia sheria kukabiliana na Watu wanaojihusisha na vitendo vya aina hii, na kuwa hatua madhubuti zitaendelea kuchukuliwa ili kuhakikisha haki inatendeka na vitendo vya uhujumu wa uchumi vinadhibitiwa.

Kamanda wa KmKm Pemba, Bakar Salum Othman, amewaasa Wananchi kujihusisha na kazi za halali na kuepuka vitendo vya Magendo vinavyohujumu Uchumi na kutoa Wito kwa Mamlaka husika kushirikiana na KmKm kufanikisha hilo.

Wakuu wa Taasisi za Serikali wameahidi kuendelea kusimamia sheria na taratibu zilizowekwa ili kulinda rasilimali za Taifa.

 

Imesisitizwa kuwa ulinzi wa rasilimali za Taifa na Uchumi wa Zanzibar utadumishwa kwa ushirikiano wa Wananchi na Vyombo vya Dola. hatua za kisheria dhidi ya wahalifu zitaendelea kuchukuliwa kwa nguvu na Serikali haitavumilia vitendo vyovyote vya kuhujumu Uchumi.

 

Simplenews subscription

The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.