WANAWAKE WAHIMIZWA KUSIMAMIA MALEZI

SIKU YA WANAWAKE DUNIANI
English

Baada ya kufanikiwa kiuchumi Wanawake Nchini wameaswa kuzingatia mila na desturi zinazojenga na sio kubomoa na kuharibu kizazi cha baadae

Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Mkoani Geita kilopambwa na ujumbe mzito wa kuwataka Wanawake Nchini kuoanisha mafanikio ya kiuchumi na utunzaji wa mila na desturi bora.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi maalum, Dkt. Dorothy Gwajima, amesisitiza kuwa juhudi za Serikali za kumuinua Mwanamke kiuchumi hazina lengo la kubomoa misingi ya Familia, bali ni kupunguza ukatili Majumbani.

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto kutoka Zanzibar, Ndg . Zawadi Nassor, ametoa rai kwa Wanawake kutodharau nafasi ya Mwanaume ndani ya Familia wakati wakidai haki zao.

Katika hatua nyingine ya kihistoria, Mkoa wa Geita umezindua Mradi wa pamoja, unaolenga kutokomeza ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto.

Mradi huu unaofadhiliwa na Benki ya Dunia kwa thamani ya Shilingi Bilioni 262, unatekelezwa katika Mikoa 10 na Halmashauri 40 Nchini ili kutoa ulinzi wa kudumu kwa makundi hayo.

 

Simplenews subscription

The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.