English
Kamishna wa Kikosi cha Zimamoto na Uokozi Zanzibar Rashid Mzee Abdallah amesema Kikosi hicho kinaendelea kujiimarisha kwa kuwa na Vifaa vya kisasa vya kukabiliana na Majanga ya Moto.

Kamishna Rashid ameyasema hayo baada ya kupokea Gari Tisa za Kuzimia Moto na Boti moja kutoka Nchini Austria.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake Kilimani baada ya kupokea Gari hizo kupitia Bandari ya Malindi Zanzibar, Kamishna Rashid amesema miongoni mwa Gari hizo zina uwezo wa kufanya uokozi kwenye Majengo marefu na Boti itatumika kwa uokozi wa Baharini.
Kamishna huyo wa Kikosi cha Zimamoto na Uokozi amewataka Wananchi kutoa ushirikiano kwa Kikosi hicho na kuripoti matukio ya ajali za moto kwa wakati zinapotokea ili kuepuka Maafa makubwa.

