MAPIPA 88 YA DIZEL YAKAMATWA YAKISAFIRISHWA KIMAGENDO

MAFUTA MAGENDO
English

Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Mgeni Khatib Yahya, amewatahadharisha Wananchi wanaotumia Bandari Bubu  kufanya magendo kuacha vitendo hivyo, kwani Serikali haitasita kuchukua hatua kali za kisheria dhidi yao.

Akizungumza na Vyombo vya Habari kufuatia kukamatwa kwa Mapipa 88 ya Mafuta aina ya Dizeli yaliyoingizwa kinyume na sheria katika Bandari bubu ya Msuka, Wilaya ya Micheweni, Mkuu huyo wa Mkoa amesema Serikali ya Mkoa imejipanga kudhibiti matumizi ya Bandari bubu ili kudhibiti magendo.

Kamanda wa Kikosi maalum cha kuzuia magendo Kamandi ya Pemba, Ndg. Bakar Salum Othman, amesema mipaka ya Bahari ya Pemba itaendelea kuimarishwa ili kumaliza vitendo vya magendo na kulinda rasilimali za Taifa.

Naye Kamanda wa Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu wa Uchumi Mkoa wa Kaskazini Pemba Nassor hassan Nasir amesema uchunguzi wa shauri hilo utafanyika kwa haraka ili kubaini wote waliohusika na kuwachukulia hatua kali za kisheria.

 

Simplenews subscription

The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.