Waziri Wa Fedha Na Mipango Dkt. Malik Akili Amesema Sekta Ya Fedha Ni Moja Ya Eneo Litakalofanya Uchumi Wa Zanzibar Kuwa Endelevu Kama Ilivyoainishwa Katika Dira Ya Maendeleo Ya 2050.
Dkt. Malik Ameyasema Hayo Katika Ufunguzi Wa Tawi La Benki Kcb Mkunazini Zanzibar.
Katika Ufunguzi Wa Benki Hiyo, Dkt. Malik Amesema Sera Hiyo Inalenga Kuwepo Na Mageuzi Ya Kiuchumi Kwa Kuhakikisha Watu Wote Wanajumuishwa Katika Masuala Ya Kifedha Ikiwemo Huduma Za Kibenki.
Dkt. Malik Amesema Kuwepo Wa Benki Hiyo Hapa Zanzibar, Kutarahisisha Unafuu Wa Huduma Za Kifedha Kwa Ajili Ya Kutekeleza Miradi Ya Kimkakati Ya Serikali.
Mkurugenzi Mkuu Wa Benki Ya Kcb Tanzania, Cosmas Kimario Amesema Maendeleo Yanayoendelea Kutokea Katika Sekta Ya Fedha Yanatokana Na Ushirkiano Mzuri Wanaoupata Kutoka Serikalini Kwa Kuweka Mazingira Wezeshi Ya Biashara.
Meneja Wa Tawi La Kcb Zanzibar, Mbarouk Mbarouk Amesema Imekuwa Ikiendesha Program Mbalimbali Za Kukuza Mitaji Kwa Wajasiriamali Ili Kujikuza Kiuchumi.
