JAMII YA WAFUGAJI WA CHALINZE WAMETAKIWA KUWAJIBIKA KWA KUWA WALINZI ILI KUZUIA WIZI WA MIFUGO

Jamii ya wafugaji

     Jamii ya wafugaji wilayani Chalinze wametakiwa kuwajibika kwa kuwa walinzi wa kwanza wa mifugo yao ili kuzuia wimbi la wizi wa mifugo.

      Hayo yamesemwa na Mkuu wa Kikosi cha Kuzuia wizi wa mifugo (STPU) Mkoa wa Pwani, Mkaguzi wa Polisi Ally Masimike alipokua akitoa elimu ya kuzuia wizi wa mifugo kwa wafugaji na wafanyabiashara wa nyama katika mnada wa Chamakweza, Wilayani Chalinze, Aprili 24,2024.

      Masimike alieleza kuwa wizi wa mifugo unaweza kufanyika mifugo ikiwa nyumbani, malishoni au katika minada hivyo ni wajibu wa kila mfugaji kuhakikisha popote ilipo mifugo yake kuna uangalizi wa karibu ili kuzuia wizi wa mifugo hiyo kutokea.

     Kwa upande wake Polisi kata ya Vigwaza, Mkaguzi msaidizi wa Polisi Michael Millinga aliwataka wafugaji kufika mahakamani kutoa ushahidi endapo wakifungua kesi za wizi wa mifugo na ili watuhumiwa wachukuliwe hatua stahiki na kuwa fundisho kwa wengine wenye tabia kama hizo.

      Aidha wafugaji walihimizwa kuwa na mahusiano mazuri na jamii zinazowazunguka kwa kuepuka kulisha mifugo yao kwenye mashamba ya wakulima ambayo huweza kupelekea migogoro isiyokuwa ya lazima.

 

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.