AMANI NA UTULIVU KUONGEZA FURSA ZA KIUCHUMI

ZIPA

      Mamlaka Ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar Zipa imekutana Na Ujumbe Kutoka Chuo Cha Ulinzi Taifa Ndc kwa Zira Ya Kujifunza.

        Akizungumza na Ujumbe Huo Mkurugenzi Mipango Na Utafiti  Alhaj Mtumwa Jecha Amesema, Zipa inajivunia Amani iliopo Nchini kama Ajenda inayoifanya kuitangaza Nchi Duniani kote kupitia fursa zilizopo

       Amesema Hatua hiyo imesababisha Serikali kupunguza mitaji Ya uwekezaji hasa katika Kisiwa Cha Pemba pamoja na kufanya Mapitio ya Sheria ya Uwekezaji ili Kuimarisha Baadhi ya Maeneo Yenye Miradi na Kumpa Fursa ya Muekezaji Mzawa na Diaspora Kuekeza Nchini 

     Mkufunzi Mwandamuzi Wa Chuo hicho Brigedia Jenerali Chales James Ndiege Amesema kukua kwa Uchumi wa Nchi kunategemea Usalama wa Nchi, Hivyo Zipa kwa Mujibu wa majukumu yake ihakikishe Uwekezaji unaoekezwa unakuza Uchumi Wa Nchi na Kuongeza Pato la Wananchi

     Ziara Hiyo ni kati ya Mafunzo ya Vitendo na Wanafunzi Wanapata Fursa ya Kutembelea Maeneo mbali mbali kwa Kujifunza  Ambapo Miongoni mwa Wanafunzi hao Ni Kutoka Tanzania ,Ethiopia, India, Zambia, Zimbambwe Na Botswana

 

Tags
stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.