SMZ NA SMT KUTOA ELIMU YA MUUNGANO KWA WANANCHI.

MHE. HAMZA HASSAN JUMA
English

Waziri Wa Nchi Ofisi Ya Makamu Wa Pili Wa Rais Sera Uratibu Na Baraza La Wawakilishi Mhe Hamza Hassan Juma Amesema Muungano Wa Tanganyika Na Zanzibar Ndio Tunu Pekee Ya Watanzania Inayowaweka Pamoja Katika Kuimarisha Maendeleo.

Akizungumza Katika Kikao Cha Ushirikiano Baina Ya Ofisi Ya Makamu Wa Pili Wa Rais Zanzibar Na Ofisi Ya Makamu Wa Rais Tanzania Kwa Ajili Ya Kujadili Masuala Ya Muungano Na Yasiyo Ya Muungano Waziri Hamza Amesema Watanzania Wanapaswa Kuutumia Muungano Kama Ni Fursa Katika Kukuza Uchumi Ujamaa Na Ulinzi Kwa Kupitia Sekta Mbalimbali Ikiwemo Michezo.

Naibu Waziri Ofisi Ya Makamu Wa Rais Muungano Na Mazingira Mhe. Dkt Festo John Dugange Amewataka Watendaji Wa Serikali Ya Mapinduzi Ya Zanzibar Na Serikali Ya Jamuhuri Ya Muungano Wa Tanzania Waendelee Kushirikiana Katika Masuali Mbalimbali Ya Muungano Na Yasiyo Ya Muungano Jambo Ambalo Litachangia Kupunguza Gharama Za Kiutendaji.

Katibu Mkuu Ofisi Ya Makamu Wa Pili Wa Rais Dkt Islam Seif Salum Amesema Kikao Hicho Ni Moja Kati Ya Uwajibikaji Wa Taasisi Za Smz Na Smt Katika Kuhakikisha Elimu Ya Muungano Inawafikia Wananchi Wote Ili Waweze Kunufaika Na Matunda Ya Muungano.

 

Simplenews subscription

The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.