Serikali Ya Mapinduzi Ya Zanzibar Itaendelea Na Azma Yake Ya Kujenga Uchumi Shindani Na Jumuishi Kwa Kuifanya Zanzibar Kuwa Sehemu Rafiki Ya Biashara Na Uwekezaji Kwa Kuweka Miundombinu Imara, Sera Bora Na Huduma Zenye Ufanisi.
Makamu Wa Pili Wa Rais Wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla Akifungua Mkutano Mkuu Wa 17 Wa Jumuia Ya Kitaifa Ya Wafanyabiasha Zanzibar Zncc Kwa Niaba Ya Rais Wa Zanzibar Na Mwenyekiti Wa Baraza La Mapinduzi Mhe.Dkt Hussein Ali Mwinyi Amesema Serikali Kwa Kushirikiana Na Sekta Binafsi Imeimarisha Sera Za Uwekezaji, Na Kurahisisha Taratibu Za Usajili Wa Biashara Na Uwekezaji
Aidha, Amesema Serikali Imedhamiria Kuchukua Hatua Madhubuti Kama Vile Kuimarisha Uendeshaji Na Ufanisi Wa Bandari, Kuimarisha Matumizi Ya Tehama Katika Utoaji Wa Huduma, Kuimarisha Uhakika Wa Huduma Ya Nishati Pamoja Na Kuweka Mazingira Ya Biashara Na Utendaji Wa Serikali.
Waziri Wa Kazi Na Uwekezaji Ambae Pia Ni Kaimu Waziri Wa Biashara Na Maendeleo Ya Viwanda Mhe. Sharif Ali Sharif Amesema Serikali Inatambua Kuwa Sekta Binafsi Ndio Injini Ya Biashara Nchini Jambo Linalochangia Ukuwaji Wa Uchumi Na Uwekezaji Zanzibar.
Mwenyekiti Wa Jumuiya Ya Kitaifa Ya Wafanyabiashara Ali Amour Suleiman Amesema Licha Ya Mafanikio Lakini Bado Jumuiya Hio Inakabiliwa Na Matatizo Mbali Mbali Ikiwemo Kukosekana Kwa Umeme Wa Uhakika Na Kuzorota Kwa Ufanisi Wa Bandari Za Zanzibar.
