SERIKALI INAENDELEA KUWEKEZA KWENYE MIUNDOMBINU YA SEKTA YA ELIMU

Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali inaendelea kuwekeza kwenye miundombinu ya sekta ya elimu ili kuwawezesha vijana kusoma fani tofauti ndani ya Nchi.

 Rais wa Zanzibar ameyasema hayo katika mahafali ya 19 ya Chuo kikuu cha Taifa cha Zanzibar SUZA na kuwatunuku vyeti, stashahada, shahada, shahada za uzamili na uzamivu kwa wahitimu wa Chuo hicho kwa mwaka wa masomo 2022/2023, huko Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja.

DK. SHEIN AMEITAKA SERIKALI YA ZANZIBAR KUWASOMESHA WAFANYAKAZI WA KADA MBALIMBALI

Rais Mstahafu wa awamu ya saba wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein ameitaka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuwasomesha wafanyakazi wa kada mbalimbali wakiwemo wa afya ili waweze kutoa huduma bora kwa Wananachi.

Ameyasema hayo mbuzini wilaya ya magharib a katika ufunguzi wa Hospitali ya wilaya ikiwa ni shamra shamra ya maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi Zanzibar.

ARSENAL YASHUSHWA KILELENI BAADA YA MICHEZO YA JANA YA EPL

Arsenal imekosa nafasi ya kurejea kilele mwa Ligi ya Premia siku ya Alhamisi, kwa kukubali kufungwa 2-0 na West Ham huku Tottenham ikilala kwa mabao sita dhidi ya Brighton.

Washika Bunduki wa Mikel Arteta walikuwa juu ya mti wakati wa Krismasi kwa mwaka wa pili mfululizo wakiwafuata viongozi Liverpool kwa pointi mbili katika nusu ya msimu.

Washindi wa pili wa mwaka jana walimiliki mpira Emirates lakini walikosa makali dhidi ya wageni wenye nidhamu, ambao Tomas Soucek na mchezaji wa zamani wa Arsenal Konstantinos Mavropanos waliwafungia mabao.

BINGWA MTETEZI MICHUANO YA MAPINDUZI CUP AANZA NA SARE

Mabingwa watetezi wa Mashindano ya Mapinduzi Cup, timu ya Mlandege imeshindwa kutamba mbele ya Azam FC ambao ndio mabingwa wa kihitoria wa michuano baada ya kutoka sare ya bila ya kufungana katika mchezo wa ufunguzi wa Mashindano hayo kwa msimu huu, katika Uwanja wa New Amaan Complex.

Dakika 45 za kipindi cha kwanza kilikua na vuta nikuvute kwa timu zote mbili, huku lango la Azam FC likionekana kushambuliwa sana katika dakika 45 za kipindi za kipindi cha pili, na kupelekea dakika 90' zikamilike kwa sare tasa ya bila ya kufungana.

Subscribe to
 

Simplenews subscription

The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.