DKT. MWINYI ATEMBELEA MJI WA AFCON FUMBA

DKT.MWINYI
English

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameutembelea mradi wa Mji wa Afcon Fumba uliopo Mkoa wa Mjini Magharibi.

Katika Ziara hiyo Dkt. Mwinyi amembatana na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Riziki Pembe Juma, pamoja na Wadau wa Mradi wa Afcon Fumba Zanzibar.

Dkt. Mwinyi amekagua Maeneo mbalimbali ya Uwanja huo wa kisasa wa Afcon unaojengwa na Kampuni ya Orgun Group ya Uturuki, unaotarajiwa kutumika kwa michuano ya Afcon Mwaka 2027 itakayofanyika kwa ushirikiano wa Nchi Tatu za Afrika Mashariki: Kenya, Uganda na Tanzania.

Aidha, Rais Dkt. Mwinyi ametembelea na kukagua miundombinu inayotarajiwa kujengwa kuzunguka Uwanja huo, ikiwemo Hospitali, Barabara, Migahawa, Maduka makubwa pamoja na huduma nyingine muhimu zitakazouzunguka mji huo wa kisasa.

Uwanja huo unakadiriwa kuchukua Watazamaji Elfu 35, ukiwa na viwango vya ubora vinavyokubalika na shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF).

 

Simplenews subscription

The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.