WIZARA YA AFYA YAFUATILIA MATIBABU YA KIJANA ALIEUMIA KWENYE MAKACHU

DKT.SAADA MKUYA
English

Kaimu Waziri Wa Afya Zanzibar Na Waziri Wa Nchi Afisi Ya Raisi Ikulu Dkt. Saada Mkuya Salum,Amesema Serikali Kupitia Wizara Ya Afya Itaendelea Kusimamia Matibabu Ya Abdallah Bakari Aliepata Ajali Ya Kupooza Mwili Ili Kuona Anarudi Katika Hali Yake Ya Kawaida.

Akizungumza Wakati Alipomtembelea Kijana Huyo Na Kuangalia Maendeleo Yake Huko Nyumbani Kwao Jang’ombe,Dkt.Saada Amesema Tokea Kutokea Kwa Ajali Hiyo Serikali Imekuwa Ikichukua Hatua Stahiki Ili Kuona Matibabu Ya Kijana Huyo Yanakwenda Kama Yanavyoelekezwa Na Wataalamu.

Amesisitiza Kuwa Serikali Itaendelea Kuchukua Hatua Zaidi Kwa Kijana Huyo Hasa Katika Kuhakikisha Anafanikiwa Kupata Ratiba Ya Mazoezi Ya Kitaalamu Ya Mwili Kama Ilivyoshauriwa Na Madaktari Wa Kijana Huyo Kwa Lengo La Kumsaidia Kurudi Katika Hali Yake Ya Awali.

Akitoa Maelezo Ya Kitaalamu Ya Kijana Huyo Mkurugenzi Mkuu Wizara Ya Afya Zanzibar Dkt. Amour Suleiman Mohamed, Amesema Kwa Mujibu Wa Ripoti Ya Kitaalamu Ya Kijana Huyo Imeonesha Kuwa Mpishano Wa Baadhi Ya Pigili Za Uti Wa Mgongo Zilizosababisha Kuathiri Mshipa Wa Hisia Jambo Lililosababisha Kukosekana Kwa Hisia Mwilini.

Nae Abdallah Bakari Amezipongeza Juhudi Zinazoendelea Kuchukuliwa Na Serikali Na Baadhi Ya Wataalamu Wa Afya Ambazo Zimesaidia Hadi Sasa Kuanza Kuinua Baadhi Ya Viungo Vya Mwili Wake Ikiwemo Mikono Jambo Ambalo Mwanzo Lilishindikana. 

Mama Mzazi Wa Kijana Huyo Abeda Nassor Saidi, Ameishukuru Serikali Hasa Kwa Viongozi Mbalimbali Wanaojitokeza Kuendelea Kumtembelea Kijana Wake.

 

Simplenews subscription

The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.