Kwa Mujibu Wa Takwimu Zilizotolewa Na Ofisi Ya Mtakwimu Mkuu Wa Serikali Ya Zanzibar, Katika Iftar Hiyo, Wanaume Waliohudhuria Walikuwa 18, 771 Sawa Na Asilimia 68.6% Na Wanawake Ni 8,574 Sawa Na Asilimia 31.4%.
Hii Ni Mara Ya Kwanza Kwa Zanzibar Kuandaa Tukio La Aina Hii Ambalo Huenda Limevunja Rikodi Ya Dunia.
Iftar Hii Ya Kitaifa Imeandaliwa Kwa Pamoja Na Shirika La Utangazaji Zanzibar Zbc, Ofisi Ya Muft Wa Zanzibar Na Kamisheni Ya Utalii Zanzibar.

Rais Wa Zanzibar Na Mwenyekiti Wa Baraza La Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi Aliyekuwa Mgeni Rasmi Katika Salamu Zake Kwa Taifa Anasema Mkusanyiko Kama Huu Haujawahi Kutokea.
Rais Dkt Mwinyi Anasema Amefurahi Kuona Watu Wamejitokeza Kwa Wingi Na Maandalizi Yamekuwa Mazuri.
Rais Dkt Mwinyi Anasema Zanzibar Imeandika Historia Kwasababu Jambo Kama Hilo Halijapata Kutokea Na Hivyo Anamshukuru Mungu Kwa Kuwawezesha Licha Ya Mvua Kunyesha Na Kwamba Hiyo Ni Ishara Ya Kwamba Mwenyezi Mungu Alikuwa Pamoja Nao Katika Jambo Hilo La Kheri.
Mkurugenzi Mkuu Wa Shirika La Utangazaji Zanzibar Ramadhan Bukini Anasema Tukio Kubwa Kama Hili La Kufutarisha Maelfu Ya Watu Lisingeweza Kufanyika Kama Nchi Haina Amani Na Utulivu.

Bukini Amempongeza Na Kumshukuru Rais Wa Zanzibar Dkt Hussein Ali Mwinyi Kwa Uongozi Wake Wa Busara Unaoifanya Zanzibar Kuwa Kisiwa Cha Amani Kwa Matukio Makubwa Yenye Minasaba Ya Kuvutia Utalii Halal Hapa Nchini.
Katibu Mtendaji Wa Kamisheni Ya Utalii Zanzibar Arif Abbas Manji Anasema Kwenye Maandalizi Ya Iftar Hii Ya Kitaifa, Waliandaa Vyakula Vya Watu Ishirini Na Tano Elfu Na Vyote Vilipata Watu Na Kumalizika.

Wadhamini Wakuu Wa Iftar Hii Ni Benki Ya Watu Wa Zanzibar- Pbz Ambao Wamekuwa Washirika Wakubwa Wa Zbc Na Matukio Makubwa Ya Kitaifa.
Tukio Hili La Kwanza La Iftar Ya Kitaifa Limehudhuriwa Na Viongozi Mbambali Wa Serikali Wa Ngazi Zote, Ofisi Ya Muft Mkuu Wa Zanzibar, Viongozi Wastaafu, Vyama Vya Siasa Na Wananchi Wa Dini Zote.
Mitandao Mbalimbali Ya Kijamii Inaonesha Kwamba Tukio Kama Hili Limefanyika Huko Beirut Lebanon Mwaka 2025 Ambapo Watu Karibu 5,800 Walikusanyika Kupata Futari Wakati Wa Ramadhan.
Kwa Tukio La Tarehe 7 Machi 2025 Huko Zanzibar La Kuandaa Iftar Ya Watu 27,345 Huenda Likawa Ndo Tukio La Kwanza Na Kubwa Zaidi Duniani.
