NDANI YA SIKU 100 WIZARA TUMEFANIKIWA KUTOA AJIRA 2,300

atibu Mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar, Dkt. Mngereza Mzee Miraji
English

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar, Dkt. Mngereza Mzee Miraji, ameeleza utekelezaji wa majukumu ya Wizara ya Afya kuanzia ngazi ya msingi hadi ngazi ya juu ya rufaa, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha mfumo wa huduma za afya Zanzibar.

Ndani ya siku 100 za utekelezaji, Wizara imefanikiwa kuajiri wahudumu wa afya ngazi ya jamii 2,300, hatua iliyopanua upatikanaji wa huduma za afya mashinani, sambamba na kuhakikisha mishahara inalipwa kwa wakati kutokana na uongozi na maelekezo ya Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi.

Aidha, Wizara imeweka mkakati maalum wa ajira kwa kushirikiana na Kamati za Masheha ili kuboresha uwajibikaji na ufanisi wa watumishi, pamoja na kukamilisha ujenzi wa Hospitali ya Lumumba na kuimarisha usimamizi wa wataalamu na vifaa vya kisasa.

Hatua nyingine muhimu ni kuwajengea uwezo vijana 20 wa Kizanzibari kupitia mafunzo ya usimamizi wa hospitali ndani na nje ya nchi, pamoja na kuweka mifumo endelevu ya mafunzo kwa madaktari na watumishi wa afya kwa kushirikiana na sekta binafsi na utumishi wa umma, ikiwa ni dhamira ya Serikali kuhakikisha huduma bora, endelevu na zenye viwango vya kimataifa kwa wananchi wa Zanzibar.

 

Simplenews subscription

The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.