SMZ IMEFANYA MAPINDUZI MAKUBWA KWENYE SEKTA YA AFYA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar, Dkt. Mngereza Mzee Miraji
English

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar, Dkt. Mngereza Mzee Miraji, ameeleza kwa kina dira ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ya kuiondoa Zanzibar katika utegemezi wa rufaa za matibabu nje ya nchi na badala yake kuijenga kuwa kitovu muhimu cha huduma za afya katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Dkt. Miraji amesema Serikali tayari imewekeza zaidi ya shilingi bilioni 120 hadi 130 katika kuboresha miundombinu ya afya, huku juhudi zikiendelea kupitia mpango mkubwa wa uwekezaji unaokadiriwa kufikia zaidi ya shilingi trilioni 1.016. Lengo kuu la uwekezaji huo ni kuimarisha ubora wa huduma za matibabu, kupunguza gharama kwa wananchi wanaolazimika kusafiri nje ya nchi, na kuongeza upatikanaji wa huduma za kibingwa ndani ya Zanzibar.

Amefafanua kuwa uwekezaji huo unahusisha miradi kadhaa ya kimkakati, ikiwemo ujenzi wa Hospitali ya Rufaa pamoja na Chuo cha Binguni, ambavyo tayari vimefikia hatua za mwisho za kupata idhini. Vilevile, Serikali inaendelea na ukarabati na upanuzi wa Hospitali ya Mnazi Mmoja, ambayo sasa itakuwa na zaidi ya vitanda 200 pamoja na huduma za kisasa zitakazoongeza uwezo wa hospitali hiyo kuhudumia wagonjwa kwa ufanisi zaidi.

Kwa upande mwingine, Dkt. Miraji amesema Serikali imekamilisha ujenzi wa hospitali nne za mikoa katika visiwa vya Pemba na Unguja, hatua inayotarajiwa kusogeza huduma za afya karibu zaidi na wananchi. Aidha, kuna mpango wa kujenga kliniki maalum za matibabu ya magonjwa ya kansa zitakazogharimu zaidi ya shilingi bilioni 120, ili kukabiliana na ongezeko la magonjwa yasiyoambukiza na kupanua wigo wa huduma za kibingwa.

 

Simplenews subscription

The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.