MADIWANI MBULU WATAKA WASIOCHANGIA CHAKULA SHULENI WACHUKULIWE HATUA

Baraza la madiwani wa halmashauri ya mji wa Mbulu mkoani Manyara
English

Baraza la madiwani wa halmashauri ya mji wa Mbulu mkoani Manyara wameiomba Serikali  kuwachukulia hatua kali za kisheria Wazazi wasiochangia chakula kwa watoto wao shuleni ili kuwezesha watoto kupata chakula cha mchana na kuinua kiwango cha taaluma.


Madiwani hao Wametoa Ombi hilo wakati wa kikao cha kwanza cha baraza hilo ambapo wamelalamikia tabia ya baadhi ya wazazi kutochangia mchango wa chakula shuleni kwa watoto wao hali inayokuwa kikwazo kwa jitihada za kuinua taaluma na kuondokana na utoro shuleni.

Akijibu hoja hizo, mkuu wa wilaya ya Mbulu Michael John Semindu, ameahidi kufanyia kazi suala hilo, na kusema  kuwa moja ya mafanikio ya lishe katika Wilaya ya Mbulu ni uwepo wa chakula shuleni na kuwasihi wazazi kutekeleza wajibu wao kwa watoto ili uongeza ufahulu wao.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mbulu  Rehema Bwasi ametoa rai kwa kamati za shule,pamoja na watendaji wa vijiji wanapokuwa kwenye mikutano yao kuhakikisha wanahamasisha  kikamilifu na kuhakikisha chakula kinapatikana shuleni. Wazazi na walezi Kuchangia chakula cha mchana shuleni kwa watoto wao ni sehemu ya mchango wao katika kuinua kiwango cha taaluma shuleni.

 

Simplenews subscription

The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.