MADIWANI MBULU WATAKA WASIOCHANGIA CHAKULA SHULENI WACHUKULIWE HATUA
Baraza la madiwani wa halmashauri ya mji wa Mbulu mkoani Manyara wameiomba Serikali kuwachukulia hatua kali za kisheria Wazazi wasiochangia chakula kwa watoto wao shuleni ili kuwezesha watoto kupata chakula cha mchana na kuinua kiwango cha taaluma.
Madiwani hao Wametoa Ombi hilo wakati wa kikao cha kwanza cha baraza hilo ambapo wamelalamikia tabia ya baadhi ya wazazi kutochangia mchango wa chakula shuleni kwa watoto wao hali inayokuwa kikwazo kwa jitihada za kuinua taaluma na kuondokana na utoro shuleni.
