Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mbunge wa Jimbo la Chaani, Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud, ameendelea kuimarisha uhai wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kukamilisha ukarabati wa matawi mawili kwa kupiga plaster, huku tawi la Ketwa likiwa hatua za mwisho.
Mhe. Ayoub alizungumza hayo katika mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika visiwani Zanzibar, ambapo alibainisha kutenga shilingi milioni 20 kwa ajili ya mashindano ya Qur'an ya jimbo ili kuimarisha umoja wa wananchi wa Chaani.

Katika sekta ya Maji, Mbunge huyo amewekeza zaidi ya shilingi milioni 13 kwenye mpango wa ujenzi wa matanki manne, visima nane, na mabomba ya kilomita 40 katika jimbo zima. Kwa sasa, tayari amekamilisha uimarishaji wa visima na ugawaji wa matanki ya maji katika shehia za Chaani Masingini, Mcheza Shauri, Kikobweni, Kinyasini, na Badamaji ili kuwahakikishia wananchi huduma hiyo muhimu kwa vitendo.
