Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Zanzibar imewakamata Watuhumiwa Watatu wanaosadikiwa kusambaza na kuuza Dawa za kulevywa kwa kutumia mbinu mpya ambayo ni kuchanganya na Dawa za Binaadamu
Akitoa Taarifa kwa Waandishi wa Habari Ofisini kwake Migombani Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Zanzibar Kanali Burhani Zubeiri Nassoro amesema bidhaa hizo zenye vifungashio zimekamatwa katika Maduka mabali mbali hapa Zanzibar
Katika Opresheni hiyo wamekamata Pipi , Choklat, Korosho na Shisha zenye Majina ya Elfbar na Freshy ndani yake zikiwa na Bangi, Cocaine na lsd zikiwa na uzito wa Kilo 7 Nukta 448.



Dawa hizo zimeingizwa na Raia wa Romani anaye fahamika kwa Jina la Alexandru Rozescu, Mkaazi wa Mbweni akizisambaza katika Nchi mbali mbali.
Akiwataja Watuhumiwa wengine ni Nahid Bàndar na Farhad Mustafa Gulam wote ni Raia wa Tanzanian wenye asili ya India.

Amesema walengwa wa Dawa hizo ni Watoto chini ya Miaka 18 na Vijana ambao ni tegemeo la Taifa hivyo amewaomba Wazazi na Walezi kuwa na tahadhari ya Watoto wao kwani Dawa hizo zinasababisha Madhara Makubwa
