SERIKALI ITAENDELEA KUJENGA UCHUMI JUMUISHI

Serikali Ya Mapinduzi Ya Zanzibar Itaendelea Na Azma Yake Ya Kujenga Uchumi Shindani Na Jumuishi Kwa Kuifanya Zanzibar Kuwa Sehemu Rafiki Ya Biashara Na Uwekezaji Kwa Kuweka Miundombinu Imara, Sera Bora Na Huduma Zenye Ufanisi.

RAIS SAMIA AMESISITIZA VIPAUMBELE VYENYE UMUHIMU KWA TANZANIA NA AFRIKA

Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Watanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan Amesisitiza Vipaumbele Vyenye Umuhimu Kwa Tanzania Na Afrika Kwa Ujumla, Ikiwemo Ustahimilivu Wa Majanga, Uendelevu Wa Madeni, Mpito Wa Haki Wa Nishati Safi, Uongezaji Thamani Wa Madini Muhimu, Na Usalama Wa Chakula.

Rais Samia Ameyasema Hayo Katika Mkutano Wa 39 Wa Wakuu Wa Nchi Na Serikali Wa Umoja Wa Afrika (Au) Unaoendelea Jijini Addis Ababa Ethiopia.

MHE. AYOUB AANZA UTEKELEZAJI WA AHADI NNE ZA MAENDELEO JIMBO LA CHAANI

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Chaani, Ayoub Mohammed Mahomud ameweka bayana dhamira yake ya kuleta mapinduzi ya kiuchumi jimboni humo kwa kutangaza kuanza kwa utekelezaji wa ahadi zake nne kuu alizozitoa wakati wa kipindi cha kampeni.

​Akizungumza leo na Wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kisauni, Mbunge huyo amesisitiza kuwa kipaumbele chake cha kwanza ni Usalama wa Chakula, akilenga kuhakikisha jimbo hilo linakuwa na akiba ya kutosha ya chakula isiyopungua tani 100 kila mwaka.

VYOMBO VYA ULINZI VIMETAKIWA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAO KIKATIBA

Makamu Wa Pili Wa Rais Wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla Amesema Msingi Mkubwa Ya Wiazara Ya Mambo Ya Ndani Ya Nchi Ni Kuhakikisha Inalinda Wananchi Na Mali Zao Pamoja Na Kutenda Haki Kwa Raia Wa Jamuhuri Ya Muungano Wa Tanzania.

Akizungumza Na Uongozi Wa Wizara Ya Mambo Ya Ndani Ya Nchi Uliofika Ofisini Kwake Baraza La Wawakilishi Chukwani Zanzibar Kwa Ajili Ya Kujitambulisha Amesema Suala La Usalama Wa Raia Na Mali Zao Ni Muhimu  Katika Kuimarisha Nchi Kisiasa,  Kiuchumi Na Kijamii 

KISWAHILI CHATAMBULIWA KIMATAIFA

Katibu Mtendaji Wa Kamisheni Ya Kiswahili Afrika Mashariki, Dkt. Caroline Asiimwe, Amesema Kiswahili Kimepiga Hatua Kubwa Kimataifa, Kikitambuliwa Na Umoja Wa Mataifa Na Unesco Kama Lugha Yenye Mchango Muhimu Duniani.

Hatua Hiyo Inatokana Na Idadi Ya Wanaozungumza Ikiendelea Kuongezeka Barani Afrika Na Kutumika Katika Majukwaa Ya Kidiplomasia, Biashara Na Teknolojia Jambo Linalothibitisha Kuwa Si Lugha Ya Kikanda Pekee, Bali Ni Sauti Ya Afrika Katika Jukwaa La Dunia.

ZAA YAKANUSHA TAARIFA ZA WIZI WA MIZIGO UWANJA WA NDEGE WA (AAKIA)

Zanzibar, 11 Februari 2026 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar (ZAA), Ndugu Seif Abdalla Juma, ametoa ufafanuzi kwa umma kufuatia taarifa zilizosambazwa kwenye baadhi ya mitandao ya kijamii na vyombo vya habari zikidai kuwa mamlaka hiyo imeshindwa kudhibiti matukio ya wizi wa mizigo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume (AAKIA).

WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU NCHEMBA AFUNGUA UWANJA WA NDEGE WA MTEMERE

Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba leo Februari 11, 2026 amezindua uwanja wa ndege Mtemere uliopo katika kijiji cha Mloka, mkoani Pwani kwenye hifadhi ya Taifa ya Nyerere.

Uzinduzi wa uwanja huo umeenda sambamba na uzinduzi wa miradi mingine 20 (kufanya miradi 21) ikiwemo Malango ya kuingilia Hifadhini, vituo vya taarifa kwa wageni, kambi za wageni, Eneo la Kupumzikia wageni, Nyumba za wageni, Hosteli za Wanafunzi, kituo cha kufuatilia ikolojia, na vituo vya askari.

JAPAN NA ZANZIBAR ZAAHIDI KUSHIRIKIANA

Makamu Wa Pili Wa Rais Wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla Amesema Serikali Ya Mapinduzi Ya Zanzibar Itaendeleza Uhusiano Ulipo Kati Ya Serikali Ya Japan Na Zanzibar Uliodumu Kwa Muda Mrefu.

Mhe. Hemed Ameyasema Hayo Alipofanya Mazungumzo Na Balozi Wa Japan Nchini Tanzania Yoichi Mikami Afisini Kwake Vuga Zanzibar.

Amesema Uhusiano Uliopo Kati Ya Tanzania Na Japan Utaendelea Kukuza Ushirikiano Katika Pande Zote Mbili Katika Kuimarisha Sekta Za Kilimo, Biashara, Maji Safi Na Salama, Maendeleo Ya Viwanda, Utalii Na Miundombinu Mbali Mbali.

SEKTA YA FEDHA NGUZO YA UCHUMI ENDELEVU

Waziri Wa Fedha Na Mipango Dkt. Malik Akili Amesema Sekta Ya Fedha Ni Moja Ya Eneo Litakalofanya Uchumi Wa Zanzibar Kuwa Endelevu Kama Ilivyoainishwa Katika Dira Ya Maendeleo Ya 2050.

Dkt. Malik Ameyasema Hayo Katika Ufunguzi Wa Tawi La Benki Kcb Mkunazini Zanzibar.

Katika Ufunguzi Wa Benki Hiyo, Dkt. Malik Amesema Sera Hiyo Inalenga Kuwepo Na Mageuzi Ya Kiuchumi Kwa Kuhakikisha Watu Wote Wanajumuishwa Katika Masuala Ya Kifedha Ikiwemo Huduma Za Kibenki.

NDANI YA SIKU 100 WIZARA TUMEFANIKIWA KUTOA AJIRA 2,300

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar, Dkt. Mngereza Mzee Miraji, ameeleza utekelezaji wa majukumu ya Wizara ya Afya kuanzia ngazi ya msingi hadi ngazi ya juu ya rufaa, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha mfumo wa huduma za afya Zanzibar.

Ndani ya siku 100 za utekelezaji, Wizara imefanikiwa kuajiri wahudumu wa afya ngazi ya jamii 2,300, hatua iliyopanua upatikanaji wa huduma za afya mashinani, sambamba na kuhakikisha mishahara inalipwa kwa wakati kutokana na uongozi na maelekezo ya Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi.

Subscribe to news
 

Simplenews subscription

The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.