KAMATI YA BARAZA LA WAWAKILISHI YARIDHISHWA NA MIRADI YA UBORA UWANJA WA AAKIA
Kamati ya Baraza la Wawakilishi ya Miundombinu, Ardhi na TEHAMA imeeleza kuridhishwa na maendeleo ya miradi ya ujenzi na maboresho ya miundombinu katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume (AAKIA), ikisema miradi hiyo inakidhi viwango vya kimataifa na itachangia kwa kiasi kikubwa kukuza sekta ya usafiri wa anga na uchumi wa Zanzibar.


