Pamoja na Mvua kubwa iliyonyesha katika Visiwa vya Unguja leo, Mashindano makubwa ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur-an yamefanyika kwa ufanisi katika Uwanja wa Amani Complex.


Mashindano hayo yameongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi ambapo Mshindi wa kwanza ni Mshiriki kutoka Zanzibar.
Mapema Dkt. Mwinyi aliwasili Viwanja vya Amani Complex akiwaongoza Mamia ya Waumini waliojitokeza katika tukio hilo muhimu la kidini ambalo limewakusanya Washiriki 12 kutoka Mataifa mbalimbali Duniani.
Hawa hapa ni baadhi ya Washiriki wa Mashindano hayo.



Baada ya Mashindano hayo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi aliwahutubia Waumini wa Dini ya Kiislamu waliofika hapo, amesema Mashindano ya Dunia ya Kuhifadhi Qur-an yamekuwa kivutio kipya cha kuitambulisha Zanzibar Kimataifa kutokana na kushirkisha Washiriki kutoka Mataifa mbalimbali.
Dkt. Mwinyi amewanasihi Waumini wa Dini ya Kiislamu kufuata muongozo wa Qur-an ili kuwa na jamii bora yenye kufuata maadili pamoja na amewasisitiza Washiriki kujifunza tabia njema kwani lengo sio kupata cheti bali ni kuishi kwa nidhamu na kukuza utamaduni wa Kiislamu katika maisha yao ya Kila Siku.
Rais wa Zanzibar aliwakabidhi Vyeti na Zawadi Washindi Watatu wa Mashindano hayo pamoja na Washiriki wengine, ambapo Mshindi wa kwanza anatoka Zanzibar aliyepata Shilingi Milioni Thelathini, Mshindi wa Pili kutoka Nigeria amekabidhiwa Hundi ya Shilingi Milioni 20 na Mshindi wa Tatu anatoka Nchini Uingerza aliyepata Milioni 10.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Zanzibar Ramadhani Bukini, amesema ZBC imeanza vizuri katika kuandaa Mashindano lakini lengo kuyaendeleza zaidi.

